Mbunge wa Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI leo ametoa mabati 142 yenye thamani ya Shilingi 4,828,000/= aliyoahidi wakati wa kampeni kwa ajili ya ujenzi wa shule shikizi Mkurumuzi Kange Kata ya Maweni.
Mhe. Ummy Mwalimu amekabidhi mabati hayo mbele ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga ndugu Daudi Mayeji na viongozi wengine wa kata na mtaa wa Kange.
Mhe Ummy ameeleza kuwa katika mwezi huu April 2021, tayari Rais Samia ameleta shilingi milioni 660 kwa ajili ya kujenga madarasa na vyoo katika Shule za Msingi za Msala, Mapambano, Kasera, Jaje na Bombo na Shule za Sekondari za Kirare,Macechu,Mikanjuni, Mnyanjani na Tongoni pamoja na ujenzi wa bweni la sekondari MACECHU.
Shule ya Msingi Kange ina jumla ya wanafunzi 1,075 kuanzia darasa la awali hadi darasa la Saba. Kwa mwaka 2021 wanafunzi wa awali walioandikishwa ni 88 na darasa la kwanza ni 162. Baadhi ya wanafunzi wanatembea umbali mrefu zaidi ya km 3 hivyo kusababisha mahudhurio ya wanafunzi kuwa hafifu, Usalama mdogo wa wanafunzi hasa wa awali na darasa la kwanza.
Aidha mhe Ummy ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi wa Kange na Maweni kwa ujumla kwa kumchagua yeye kuwa mbunge wa Jimbo la Tanga, na mhe. Colyvas kuwa diwani wa kata ya Maweni na Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliekuwa Rais wa awamu wa 5 ambae Mungu amempenda zaidi .Mhe Ummy ameeleza kuwa sasa Rais Samia ameshika usukani wa nchi na hivyo hatuna budi kumuombea na kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake.
Baadhi ya wananchi walimpongeza Mhe mbunge kwa kutekeleza ahadi zake ambazo aliziahidi kwa wana Tanga Mjini. Pia kwa kuteuliwa kuwa Waziri Wa Tamisemi.
Jengo la Shule Shikizi ya Mkurumunzi.
Mje.Ummy Mwalimu akiwa kwenye Kikao na Wananchi wakati wa makabidhiano ya Vifaa hivyo.
Mhe.Ummy Mwalimu akikabidhi Mabati hayo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.