Baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili katika Halmashauri ya Jiji la Tanga ukitokea wilayani Pangani.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ally amezindua Mardi wa Maji uliopo Kata ya Kirare -Tundaua baada ya kuridhishwa na ukaguzi wa nyaraka zote muhimu zinazohusu mradi huo pamoja na kuhoji wananchi kuhusu upatikanaji wa maji safi .
Mradi huu wenye gharama ya zaidi ya Tsh Mil.800 ambao utahudumia wananchi wa Mwalongo,Mapojoni na Kirare.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali amezindua mradi wa kituo cha Afya Duga Jijini Tanga baada ya kuridhishwa na ujenzi unaoendelea kituoni hapo .
Awali akisoma taarifa kwa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Dr Magreth Matutu amesema Mradi huo Umegharimu kiasi cha Shilingi Mil700 ambazo ni fedha za Ruzuku kutoka Serikali kuu na Shilingi Mil 500 zimetumika katika upanuzi wa kituo hicho cha Afya na Mil 200 zitatumika katika ununuzi wa visa Tiba.
Pia katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu amesema kituo cha Afya Duga ni moja ya vitro vitano vinavyoendelea kujengwa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Tanga katika kuhakikisha Mwananchi wanapata huduma bora za Afya.
Wakati huohuo kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa matumizi matumizi ya Mapato ya ndani katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa haleta kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Mradi kiwanda cha ushonaji kwa kikundi cha vijana (TAYOTAI) Wenye umri kuanzia miaka 15-35.
Vijana hao wamesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Tanga imewapatia mkopo wa Mil.60 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa pamoja na mtaji wa kuanzisha biashara.
TAYOTAI pia wameongeza kuwa mari tuo wa ushonaji utawasaidia katika kujipatia kipato na kutekeleza kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda.
Pia Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa maendeleo yaliyopo ndani ya Jiji la Tanga ni kwa jailli ya Mwananchi hivyo ni vyema wazazi wakatumia fursa zilizopo ikiwemo kuwapeleka watoto katika kikundi hicho cha vijana ili nao waweze kujifunza na kujitengenezea kipato.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.