Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Ndg. Said Majaliwa amewataka watendaji wa kata na Mitaa kuwahudumia watu katika kutatua kero zao.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Maweni alipokwenda kuzindua mradi wa maji uliodhaminiwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Islamic Help
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Mhe. Joseph Colvas, amesema ni kwa muda mrefu wamepata changamoto ya maji hivyo ameishukuru taasisi hiyo kwa kuwaletea mradi huo wa maji pamoja na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa ya shule shikizi.
(Mwandishi: Salma Ramadhani)
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.