Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Benedicto Njau amewataka wanafunzi watakaochaguliwa kuunda timu ya Mkoa ili kushindana katika mashindano ya Umitashmta ngazi ya Taifa kwa kujituma kuthubutu na kuonyesha nidhamu wakati wote wa michezo.
Njau ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya mchezo wa Umitashmta kwa ngazi ya Mkoa wa jijini Tanga katika viwanja vya shule ya sekondari Tanga ufundi.
Aidha wanamichezo hao ambao wako 965 ikiwa kati yao wavulana ni 490 na wasichana 475 ambao watashindana katika mchezo wa mpira wa Miguu,Mpira wa Wavu,Mpira wa Pete,Riadha,Mpira wa Kengele pamoja na fani za ndani zitakazohusisha Ngoma na Kwaya.Pia wameambatana na Walimu na viongozi takribani 150 walioambatana na timu hizo kutoka Halmashauri zote za mkoa wa Tanga na wanatarajia kuchagua wanamichezo 100 pamoja na Walimu 15 watakaounda time ya mkoa kwa jailli ya kushiriki mashindano ya Taifa ambayo yatafanyika Mkoani Mtwara.
Hata hivyo kwa upande wa Mratibu wa mashindano hayo ya Umitashumta Ndugu Miraji Juma amesema kuwa kila timu ijitume ili kupata wanamichezo wenye kiwango cha juu watakaowakilisha Mkoa wetu Kitaifa.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.