Mamlaka ya Hali ya Hewa jijini Tanga imetakiwa kutoa Elimu kwa wakulima na wavuvi kwani ni muhimu katika shuguli zao na kwa kufanya hivyo watainua uchumi wa Taifa na kuongeza mchango mkubwa katika Sekta ya Uvuvi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa jiji la Tanga Daudi Mayeji alipokutana na wavuvi na wakulima katika kikao kilichoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA katika ukumbi wa Bandari jijini hapa.
Mayeji amesema kawa huwezi kuingia katika uchumi wa kati kama wananchi wako hawana Afya nzuri hivyo kwa sehemu kubwa Watanzania walio wengi hivi sasa wanakimbia kula nyaga na badala yak wanakula samaki kwani samaki ni chakula ambacho hakina madhara hivyo kutokana na hilo wakiweza kuvua vizuri kwa kuzingatia taarifa watakazokuwa wanazipata na zinawaruhusu wavuvi kuvua vizuri wataweza kuongeza afya na kuingia kwenye uchumi wa kati wakiwa na Afya njema.
"Kama jamii itakuwa na maisha ambayo si ya uhakika wakienda kuvua wanapata ajali,Uchafu wa Hali ya hewa au kupoteza maisha wakati wananchi hao wangeweza kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa kati maana yake ni kwamba ustawi wa jamii utaathirika"Ameyasema halo Mayeji.
Wakati huohuo Halmashauri ya jiji la Tanga imepokea vifaa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya vyenye thamani ya Shilingi Millioni 14 kutoka kwa kikundi cha watu zaidi ya 100 wakiwemo wa Nje ya Nchi wakishirikiana na kampuni ya Huawei.
Akikabidhiwa vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Katibu tawala wa Wilaya Faidha Salimu amesema ni vyema kukawa na ushirikiano mzuri kwa ajili ya kufuata utaratibu wa Serikali.
Kwa upende wake Mkurugenzi wa jiji la Tanga Daudi Mayeji amesema Serikali inapokea misaada yote hasa isiyo na masharti na vifaa hivyo vitatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.