• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

MAKABIDHIANO USHURU WA MAEGESHO: JIJI LA TANGA NA TARURA MKOA WA TANGA

Imewekwa: July 1st, 2022

TARURA TANGA YAKABIDHI KAZI YA UKUSANYAJI WA USHURU WA MAEGESHO YA VYOMBO VYA USAFIRI KWA JIJI LA TANGA.

Mussa Labani - Jiji la Tanga. 


Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Tanga, alhamisi Juni 30, 2022, wamekabidhi kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho ya vyombo vya usafiri (Parking fees) kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ikiwa ni utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI iliyotangaza kurudisha ukusanyaji wa ushuru wa maegesho kwa mamlaka ya Serikali za mitaa kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Ofisi kuu ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, ambapo Halmashauri imewakilishwa na Mstahiki Meya Mhe. Abdulrahman Shiloow na TARURA Mkoa wa Tanga ikiwakilishwa na Meneja wa Mkoa Mhandisi George Tarimo.

Viongozi wengine waliohudhuria Makabidhiano hayo ni pamoja na Naibu Meya Mhe. Colyvas Joseph, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Bw. Jacob Samwel, Meneja wa TARURA Wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene, baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri na TARURA.

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo, Mhandisi Tarimo amesema TARURA wapo tayari kushirikiana na Jiji la Tanga katika kufanikisha kazi ya kukusanya ushuru na kutenga maeneo ya maegesho ya vyombo vya usafiri, huku akishauri watu wa mapato wa Jiji kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa wakusanyaji kwani kunahitajika ufuatiliaji na wakati mwingine kwa kushtukuza ili kuhakiki iwapo magari yaliyopo kwenye maegesho yameingizwa kwenye mfumo.

"Katika kukusanya mapato tumekuwa tukitumia mfumo wa TeRMIS (TARURA eREVENUE MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM) ambao mnaweza kuurithi kwasasa hadi hapo baadae mtakapoamua muende vipi. Mkurugenzi uteua watu wako waje wakae na watu wetu kuanzia kesho (Ijumaa, Julai mosi), wataelekezana matumizi ya huo mfumo ili kazi ya kukusanya maduhuli ya Serikali isisimame." Amesema Mhandisi Tarimo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya Mhe. Shiloow amesema anaamini kazi hiyo itafanyika vizuri kwani sio kitu kigeni kwa Halmashauri kwa kuwa kabla ya kwenda TARURA ilitekelezwa katika ngazi ya Halmashauri.

"Sasa waswahili wanasema, mchuzi wa mbwa hunywewa wa moto, hivyo muandae utaratibu wiki hii, muwaite wale wote waliokuwa wakifanyakazi na TARURA katika kukusanya ushuru wa maegesho, mkae nao mu-update(mhuishe) taarifa zao, na kishe muendelee nao na kazi" Aliagiza Mstahiki Shiloow.

Katika makabidhiano hayo, TARURA imekabidhi mali na vifaa walivyokuwa wakitumia katika kukusanya ushuru wa maegesho zikiwemo mashine za malipo (POS) 42 ambapo kati ya hizo, mashine 15 zilikuwa zikiendelea na kazi mtaani, mashine 10 zilikabidhiwa zikiwa nzima na mashine 17 zikiwa na hitilafu.

TARURA pia imekabidhi wafanyakazi wa ajira ya muda waliokuwa wakifanya kazi hiyo, mfumo wa makusanyo, nakala ya sheria inayotumika na mkataba wa makubaliano (MoU).

Uondoaji wa kazi ya makusanyo ya maegesho (parking fees) kwa TARURA kuna lengo la kuiwezesha kujikita katika jukumu lake la msingi la ujenzi na matengenezo ya barabara na madaraja ya mijini na vijijini.

Katika kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha usafi na usalama wa miji, Ofisi ya Rais TAMISEMI ilitangaza kurejesha kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho kwa mamlaka za Serikali za mitaa kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023, ili fedha zitakazo kusanywa, sehemu yake zirudi kwenye Halmashauri ziweze kutumika kwa ajili ya kugharamia usafi wa Barabara, mifereji na uwekaji na uendeshaji wa taa za barabarani katika mamlaka husika.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.