Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloow, alhamisi Septemba 29, 2022 ameongoza mkutano maalum wa Baraza la Madiwani wa kupitia taarifa ya hesabu za mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2022 uliofanyika katika ukumbi wa limestone, jengo la ofisi kuu ya Halmashauri.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Dkt. Sipora J. Liana (PhD), amesema kwa mujibu wa sheria ya fedha Na. 9 ya mwaka 1982 pamoja na marekebisho yake na mwongozo wa fedha wa serikali za mitaa, Halmashauri ina wajibu wa kuandaa taarifa ya hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha na kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba ya kila mwaka.
Mkutano huo wa kisheria, ulihudhuriwa na viongozi wa chama na Serikali kutoka Wilaya ya Tanga, ambapo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tanga, Meja Mstaafu Hamis Mkoba alisifu umoja na ushirikiano uliopo na kwamba unasaidia maendeleo kusonga mbele.
Wajumbe wa mkutano waliipitisha taarifa hiyo kwa kauli moja, huku wakiamini kwamba Halmashauri ya Jiji la Tanga itaendelea kupata Hati safi kutokana na hesabu kuandaliwa kwa kuzingatia matakwa yote ya sheria na miongozo mbalimbali ya ufungaji wa Hesabu za Serikali.
Labani, M.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Jiji la Tanga.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.