Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wamerejea Jijini hapa baada ya kuhitimisha ziara yao ya siku nne Jijini Dodoma. Ziara hiyo ilianza kwa wao kuwasili Jijini humo Siku ya Jumatano, Februari 08, 2023.
Wakiwa Jijini Dodoma, walianza ziara yao katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kupokelewa na Naibu Meya wa Jiji hilo, Mhe. Jamal Ngalya ambaye ni Diwani wa Kata ya Kizota, na Mkurugenzi wa Jiji, Bw, Joseph Mafuru, na baadhi ya wataalamu wa Halmashauri hiyo.
Baada ya mapokezi hayo, Waheshimiwa Madiwani walipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mikubwa mitano ya kitega uchumi inayotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani, na mradi mkubwa wa barabara ya mzunguuko (ring road) unaotekelezwa na fedha za Serikali Kuu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru, ambapo miradi hiyo, inatarajiwa kuwa vyanzo vya mapato kwa Halmashauri hiyo.
Miradi iliyotembelewa na Waheshimiwa Madiwani katika ziara hii, ilihusisha:
Siku ya Ijumaa, February 10, 2023, Waheshimiwa Madiwani walihudhuria kikao cha Bunge kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ambapo walipata nafasi ya kujifunza shughuli za uendeshaji wa vikao vya Bunge, na kusikiliza Hotuba ya kuhairisha Bunge iliyosomwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Baada ya kuhairishwa kwa Bunge, Madiwani wa Jiji la Tanga walipata nafasi ya kusalimiana na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na baadhi ya Mawaziri na Wabunge, na baadae wakiwa na Mhe. Ummy Mwalimu, walifanya vikao vya kimkakati na Mawaziri Mh. Mashimba Ndaki, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, na Mhe. Dkt. Anjelina Mabula, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
Katika kipindi chote cha ziara hii, Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini ambaye pia ni Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu (Diwani kwa nafasi yake kama Mbunge) aliungana na Madiwani wenzie wa Jiji la Tanga katika muda wote wa ziara ikiwemo kuwezesha itifaki za Bungeni.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.