Mstahiki meya wa jiji la tanga Mustapha Seleboss amewapongeza Madiwani kwakusimamia mapato vizuri ya Halmashauri ya Jiji la Tanga na kupelekea kupata hati safi .
Akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Baraza la Madiwani Seleboss aliwataka Madiwani na Wananchi kuacha kutoa takwimu za ugonjwa wa Corona na badala yake kuwaachia mamlaka husika.
“Waheshimiwa Madiwani tumekuwa chachu ya kusimamia matumizi vizuri na hivyo hili ndio limepelekea kupata hati safi “Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Mbali na hayo pia Seleboss aliweza kuzipongeza jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kumtanguliza mwenyezi mungu kwa kila jambo .
“Tuone ni namna gani ya sisi Watanzania kuona tunamuunga mkono Rais Magufuli kwa kitendo cha kuwahimiza watu kumtanguliza mungu katika vitu mbalimbali hata kwa hili janga la Corona “Aliongeza hayo Mstahiki Meya Seleboss
Sambamba na hayo pia Seleboss amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa usafiri pindi janga lolote linapojitokeza .
Seleboss ameongeza kwa kuwataka Madiwani hao kushirikiana na wananchi katika kupambana na ugonjwa wa corona .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.