Mstahiki meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi amewataka Madiwani na Watendaji kuendelea kutekeleza maagizo yanayo tolewa na Rais Magufuli pamoja na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Selebosi aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha upokeaji taarifa za kata pamoja na kufanya tathimini kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.
“Kwanza nianze kwa kuwatakia pole Madiwani wote kwa janga hili la Corona ila tujue wajibu wetu sisi kama viongozi ni kusimamia na kutekeleza yale yote tunayoambiwa na kiongozi wetu Mkubwa wan Nchi hii.”Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Seleboss ameongeza kwa kuwataka wadiwani hao kufanya kazi kwa vitendo ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinaowakabili wananchi wao .
Sambamba na hayo pia Seleboss amewaomba Madiwani wakiwa kwenye kamati zao kujadili mambo ya muhimu pamoja na kufanya utekelezaji ili wakiyafikisha katika vikao vya Mabaraza ya Madiwani kufanya tathimini .
Mbali na hayo pia Seleboss akaiomba Halmashauri kurejesha utekelezaji katika kero zinazoweza kutekelezeka ndani ya bajeti .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.