Desemba 6, 2023.
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ndg Saidi Majaliwa, amekabidhi pikipiki tatu kwa Maafisa Ugani wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, zilizotolewa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuwawezesha Maafisa hao kuwafikia na wananchi katika maeneo yao.
Maafisa Ugani waliopata pikipiki hizo ni kutoka Kata za Pongwe, Kirare na Kitengo cha Uvuvi.
Akizungumza baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Mkurugenzi Majaliwa amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha watumishi kwa kuwapatia vitendea kazi, ikiwa ni pamoja na usafiri ili kuwafikia na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
Majaliwa pia amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa fedha nyingi za miradi ya maendeleo anazoleta katika Jiji la Tanga, na kwamba fedha hizo zimegusa miradi katika sekta mbalimbali.
Mkurugenzi Majaliwa amewataka Maafisa waliokabidhiwa pikipiki hizo kuzitunza na kuzitumia kwa lengo lililokusudiwa, akiahidi kufanya ufuatiliaji kuona vifaa hivyo vinatimiza lengo la kununuliwa kwake.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.