Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ametoa kompyuta 20 kwa shule za sekondari 10 zilizopo Jiji hapa kwaajili ya kurahisisha baadhi ya kazi katika shule hizo ambazo zilikuwa na changamoto ya vifaa hivyo.
Zoezi hilo limefanyika katika shule ya Sekondari Mkwakwani ambapo Walimu Sakuu wa Shule hizo kumi za Sekondari ambazo ni Mkwakwani ,Chongoleani ,Mnyanjani,Kihere ,Maweni,Mikanjuni,Mwapachu,Ndaoya ,Nguvumali na Tongoni wamekutana kwaajili ya kupokea kompyuta hizo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya kompyuta hizo katika Shule ya Sekondari ya Mkwakwani Afisa Elimu Sekondari Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa amesema kupewa kwa kompyuta hizo kutasaidia utendaji kazi mzuri .
“Tukio ambalo Waziri unalifanya kwa Muda huu sio kama litaenda kupunguza uhaba wa kompyuta tu ila italeta maendeleo kama utayarishaji wa bajeti katika Shule utaimarika ,pamoja na usajili kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza utaenda kwa haraka “,.Alisema Afisa Elimu Sekondari Lusajo Gwakisa
Nae Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji amesema atahakikisha wanafunzi 1862 waliofaulu wanapata nafasi hata ikiwa kwa kupishana kulingana na madarasa yaliyopo .
Kwa upande wake Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu amesema anaimani kompyuta hizo zitatumika vizuri kwani anaimani na Shule hizo.
“Mhe Raisi Dkt Magufuli amewekeza katika maeneo ya Elimu ,Afya na takribani karibu milioni tisini kila mwezi Serikali kuu inaleta kwaajili ya Elimu bure Tanga kwaiyo mimi katika nafasi yangu ntaendelea kuwasemea walimu wa Tanga “,.Alisema Ummy Mwalimu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto
Sambamba na kutoa kompyuta hizo Waziri Ummy pia aliweza kutembelea kituo cha ushonaji cha Tayotai na kutoa pesa kwaajili ya kuendeleza kikundi hicho na kufahamu maendeleo yake.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katoka shule ya Mkwakwani alikokabidhi kompyuta 20 kwa Shule 10 za Sekondari.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.