Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka huu, 2025, Bw. Ismail Ali Ussi, amepongeza miradi ya elimu iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2025 katika wilaya ya Tanga, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika Jumatatu ya Juni 16, 2025, akisema ni ya mfano wa kuigwa na Halmashauri zingine.
Bwana Ussi amesema katika uongozi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, maboresho makubwa yamefanyika katika miundombinu ya kufundishia na kujifunzia, ambapo sasa mazingira yamekuwa bora, akitolea mfano wa miaka 15 iliyopita, baadhi ya maeneo watoto walikaa chini na kushindwa kujifunza vizuri.
Katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu, miradi miwili ya elimu awali na msingi ilipitiwa na Mwenge wa Uhuru, ambapo mradi wa kwanza ulikuwa ni uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa ya ghorofa kwa jengo la chini, ofisi moja ya walimu pamoja na matundu 13 ya vyoo katika shule ya Msingi Mbuyuni, iliyopo kata ya Nguvumali, mradi unaogharimu kiasi cha TZS. 388,769,596.80 ikiwa ni fedha za mapato ya ndani.
Mradi wa pili ukiwa ni mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya
madarasa ya awali, matundu ya vyoo sita na uzio unaogharimu kiasi cha TZS 70,100,000.00 katika shule ya Msingi Mwakidila, iliyopo kata ya Tangasisi, ikiwa ni fedha za mradi wa Boost.
Akiwa katika shule ya Msingi Mwakidila, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru aliguswa na ubora wa mradi na shangwe la walimu wa shule hiyo ambao walipendeza kwa sare huku wakiimba nyimbo za kufurahia Mwenge wa Uhuru kuzindua mradi wao, jambo lililomfanya kiongozi huyo kutoa zawadi ya fedha taslimu kwa walimu hao.
Mwenge wa Uhuru 2025, unakimbizwa na kauli mbiu isemayo “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu’’
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.