wakina mama nchini wametakiwa kuhudhuria kliniki pindi wanapotambua kuwa na ujauzito Sambamba na kutumia vidonge vyenye madini ya Foliki asidi ili kuepukana na kujifungua watoto wenye Tatizo la kichwa kikubwa na Mgongo wazi.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee jinsia na watoto Ummy Mwalimu alipokuwa akiongoza maadhimisho ya Siku ya mtoto mwenye kichwa kubwa na mgongo wazi Duniani Yaliyofanjnya kitaifa mkoani Tanga.
Ummy amesema ni muhimu kwa kina mama kuhudhuria kliniki na kutumia vidonge hivyo kwani vinasaidia kuongeza virutubisho amba vitamsaidia mama wakati wa kujifungua .
“Maadhimisho haya yanawahamasisha wakinamama kuhudhuria kliniki mapema mara wanapojigundua ni wajawazito kwani tunalo tatizo kubwa sana wataalamu wa afya wanataka wajawazito kuhudhuria kliniki angalau ndani ya miezi mitatu baada ya kugundua kuwa ni wajawazito “,.Alisema Waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee jinsia na watoto Ummy Mwalimu
Sambamba na hilo Ummy Mwalimu alizitaka yake Halmashauri kote nchini kutumia 2% ya mapato ya ndani kwa lengo la kuwainua walemavu nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amesema Halmashauri zinatakiwa kutenga 10% kwaajili ya kuwawezesha vijana,wakina mama pamoja na walemavu .
Baadhi ya walemavu na wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi yaliyofanyika kitaifa Mkoani Tanga
waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee jinsia na watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi kwenye maadhimisho ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi yaliyofanyika kitaifa Jijini Tanga.
Maandamano kuelekea katika uwanja wa Tangamano katika maadhimisho ya siku ya mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi yaliyofanyika kitaifa Mkoani Tanga
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.