Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Bi. Hawa Msuya, leo Jumanne, Augosti 15, 2023, ameendesha vikao vya robo ya nne vya Kamati ya Lishe na Kamati ya Tathmini ya Mkataba wa Lishe Wilaya ya Tanga vilivyofanyika kwa wakati tofauti katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Katika Kikao cha Kamati ya Lishe, ambacho kimepokea na kupitia taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe katika robo ya nne ya mwaka uliyoishia Juni 30, 2023, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Bi. Msuya amewataka Wakuu wa Idara mtambuka kwenye lishe, kuhakikisha wanatenga bajeti ili kuwezesha kufanyika kwa shughuli za lishe ili kufikia malengo ya kitaifa ya uboreshaji wa lishe kwa jamii.
Bi. Msuya alitumia kikao hicho kumtambulisha Afisa Lishe mpya wa Jiji la Tanga, Bi. Rehema Kirungi ambaye amehamia hivi karibuni katika Jiji la Tanga.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Kitengo cha Lishe kwa robo ya nne ya mwaka 2022/2023, Afisa Lishe Bw. Ally Kassembo amesema Kitengo hicho kimeweza kutoa mafunzo kwa baadhi ya watumishi kuhusu utoaji nasaha kwa wagonjwa wenye upungufu wa damu, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, na masomo mbalimbali yanayohusu lishe ya mwanadamu.
Kasembo amesema moja ya mafanikio ya Kitengo hicho ni kuratibu na kusimamia bonanza la vijana, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, ambapo jumla ya watu 638 walipimwa hali zao za afya.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.