Na. Pamela Chauya
Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tanga imefanya ziara katika shule ya sekondari Ummy Mwalimu iliyopo kata ya Maweni lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na serikali katika shule hiyo ikiwa ni maelekezo ya ilani ya chama cha mapinduzi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tanga Meja mstaafu Hamisi Mkoba amesema miradi ya mabweni huwa inakumbwa na changamoto ya kushindwa kumalizika kwa wakati hivyo amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha mabweni yanakamilika kwa wakati kuruhusu wanafunzi wa kike wa kidato cha tano kuripoti shuleni hapo.
Pia mwenyekiti huyo akamtaka mstahiki Meya na Mkurugenzi kuhakikisha mwaka wa fedha unapokamilika na ujenzi wa mabweni hayo uwe umekamilika ili kuwawezesha watoto wa kike kuweza kusoma kwa utulivu huku wakikaa sehemu salama.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Abdurahaman Shiloow amepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya na amewataka watumishi kutumia vizuri fedha za serikali kwani zipo shule zimejengwa fedha sh milioni mia na zimekamilisha ujenzi huo kwa wanaosema fedha zilizoletwa hazitoshi wajitathimini
Shule ya Ummy Mwalimu ni miongoni mwa shule zilizojengwa kwa kiwango na imezingatia matumizi mazuri ya fedha na hadi sasa wametumia fedha walizopatiwa na chenji imebaki na watendaji wengine katika jiji la Tanga kujifunza kwa wezao waliofanikiwa.
Simeon Vedasto ni mchumi katika jiji la Tanga akaelezea kamati changamoto iliyosababisha kuchelewa kwa kumalizika kwa ujenzi wa mabweni katika shule ya sekondari ya Ummy Mwalimu imetoka na mashine katika mradi wa matofari kupata hitirafu na kushindwa kuzalisha matofari na kufanya baadhi ya miradi kusimama kutokana na kutokuwepo kwa matofali .
Vedasto amesema matofali yanayozalishwa na kiwanda cha Halmashauri yanatengenezwa kwa ubora na miradi yote inapata matofali hayo kwa bei nafuu.
Tunapo pata hitilafu katika kiwanda cha tofali tunatoa ruhusa kuchukua kwa wadau wengine ila changamoto inakuja ubora na bei ya matofari na usafiri mpaka kufika eneo la mradi wadau wengi wanashindwa kufikisha matofali katika eneo la mradi ndiyo huleta changamoto katika utekelezaji wa miradi yetu.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.