Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, leo Jumanne April 4, 2023 imefanya ziara ya ukaguzi wa mazingira na upangaji mji, ikiwa ni maandalizi ya kikao chake cha kawaida cha robo ya tatu ya mwaka kinachotarajiwa kufanyika alhamisi wiki ijayo.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Habib Mpa, imetembelea kiwanda cha Tanga Pharmaceutical and Plastic Limited (TPPL) kilichopo Duga, kukagua hali ya mazingira kwa ustawi na usalama wa wafanyakazi.
Kamati pia ilitembelea eneo la Tumbirini kuangalia ujenzi unaoendelea katika mradi wa vijana unaofadhiliwa na Fondation Botnar, ambapo vijana 50 kutoka kata 27 za Jiji la Tanga hujifunza ufugaji wa kuku kwa miezi sita, huku wakiwezeshwa na mradi kujikimu kwa kipindi hicho.
Kamati hiyo ambayo hukutana kila robo ya mwaka, katika ziara yake ya leo, ilipita katika eneo lenye mgogoro wa umiliki wa ardhi Mwakidila, Kituo cha mafuta cha Giga, Tangasisi na nyumba eneo la Kisosora mtaa wa Ikulu iliyojengwa barabarani na hivyo kufunga mtaa.
Ziara za Kamati huwawezesha wajumbe kuona hali halisi na hivyo kuwawezesha kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa faida ya jamii.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.