Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, leo Alhamisi Julai 20, 2023, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi na shughuli zinazotekelezwa na Idara zilizo chini ya Kamati hiyo.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Habib Mpa, imetembelea eneo la kiwanja namba 892, kitalu 'A' Kange, lililokuwa likimilikiwa na CIC ambalo kwa sasa umiliki wake umefutwa na kugawiwa kwa Chuo Cha Utumishi Kange. Kamati pia imetembelea mradi wa ujenzi wa soko la Machinga unaotekelezwa eneo la Kange karibu na kituo kikuu cha mabasi, ambao hadi kukamilika kwake, unatarajiwa kugharimu kiasi cha shillingi billion 7.7.
Ziara hii ni maandalizi ya vikao vya Kamati kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.