Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi ya Jiji la Tanga, Mhe. Al-Hajj Abdulrahman Shiloow, leo Alhamisi Julai 20, 2023, ameiongoza Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa miradi ya elimu na afya inayotekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu na Mapato ya ndani.
Ziara hiyo ilianzia katika Shule ya Sekondari ya Usagara ambapo Shule hiyo ilipokea shillingi million 450 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa Bwalo na Bweni, ambapo shillingi million 170 ni kwa ujenzi wa Bwalo la chakula, na shillingi million 280 kwa ujenzi wa Bweni.
Kamati hiyo pia ilitembelea eneo la Shule ya Msingi Jaje, panapojengwa shule mpya ya msingi kupitia fedha za mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST), ambapo mradi huo umepokea kiasi cha shillingi million 540,300,000.00 kwa ujenzi wa shule hiyo ya mikondo miwili yenye vyumba viwili vya madarasa ya elimu ya awali, pamoja na miundombinu yote ya shule ikiwemo vyoo.
Kamati ilimalizia ziara yake kwa kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Geza, iliyopo kata ya Marungu kando ya barabara kuu ya Tanga - Pangani, ambapo kiasi cha shillingi million 225 kimetolewa kutoka mapato ya ndani kwa ujenzi wa kituo hicho cha kutolea huduma za afya.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa ujenzi wa jengo la OPD (millioni 150), Nyumba ya mtumishi (million 50) na kichomea taka (million 25).
Ziara hii ni maandalizi ya kikao cha Kamati cha robo ya nne ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2023.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.