Januari 15, 2025.
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, leo Jumatano Januari 15, 2025, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Kamati cha robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2024/2025 cha kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi za Halmashauri kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2024.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Abdulrahman Shiloow, ilifika katika Hospitali ya Jiji iliyopo Masiwani, kukagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa wodi tatu (wodi ya watoto, wanawake na wanaume) ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika katika mwaka huu wa fedha.
Wodi za wanawake na wanaume, ambazo zimejengwa kisasa kulingana na mahitaji, zikiwa na uwepo wa vyumba vya kulipia (VIP), kila moja itakuwa na uwezo wa kuingia vitanda visivyopungua 24.
Kamati pia ilitembelea eneo la ujenzi wa jengo la wafanyabiashara wadogo Kange, kukagua maendeleo ya kazi hiyo, ambayo kwa sasa mkandarasi anatayarisha vyuma vya kuweka paa la jengo hilo.
Kamati ilifika shule ya msingi Mbuyuni, kata ya Nguvumali kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa la vyumba vya madarasa, ikiwa ni mpango wa Halmashauri kuanza ujenzi wa majengo ya ghorofa kwa shule zake.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.