Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ametoa rai kwa Mwananchi mmoja mmoja wa Wilaya hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na ugonjwa hatari wa corona .
Mwilapwa amesema hayo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali kwaajili ya kujikinga na ugonjwa huo kutoka kwa Ikram Ullah ambaye ni raia ya Pakistani .
Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo mwilapwa alisema kuwa ni wazi kuwa ugonjwa wa corona upo na ni hatari kama nchi haitachukua tahadhari wananchi za kutosha katika kukabiliana naugonjwa wanaweza ambukizana kwa haraka .
“Kwanza nashukuru kwa msaada ambao umeutoa kwani wanasema kutoa ni moyo wala si utajiri nimekuwa nikipokea msaada kutoka kwa makampuni mbalimbali na si mtu mmojammoja kwahiyo wewe ni wakwanza kutoa na utakuwa umewafungua macho na wengine wakatoa mmoja mmoja “Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Kwa upande wake Ikram Ullah ambaye ni raia wa pakistani alieleza sababu zilizompelekea yeye kutoa msaada huo.
“Nimeamua kutoa msaada huo ili usaidie katika kuendelea kukabiliana na ugonjwa wa corona kwani endepo tutaufumbia macho unaweza ukasambaa sana naamini hiki nilichotoa ni kidogo lakini kwa kiasi furani kitasaidia “Alibainisha hayo Ikram Ullah
Naye Ally Hamza ambaye ni Mfamasia wa Jiji la Tanga ambaye alishiriki kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga alisema vifaa hivyo vitagawanywa katika maneo stahiki huku akiwakumbusha Wananchi kuendelea kuzingatia taratibu zinazoelekezwa na wataalam wa afya .
Vifaa vilivyotolewa na Ikram Ullah ni pamoja na vitakasa mikono 315,sabuni ,groves 500 ,pamoja na barakoa 100.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.