Desemba 20, 2023.
Wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Halmashauri ya Jiji la Tanga, wamefanya kikao kazi cha kupitia Mpango Mkakati wa Halmashauri wa mwaka 2021/2022 - 2025/2026, kwa lengo la kuandaa Mpango Mkakati mpya wa Halmashauri utakao endana na mabadiliko ya kimuundo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, na malengo mapya ya Halmashauri katika kuihudumia jamii, kuongeza uwajibikaji, matumizi mazuri na sahihi ya rasirimali, n.k.
Zoezi hilo la siku nne, linaendeshwa na Mwezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa, Hombolo - Dodoma, Bw. Boaz Mbundu, ambalo mbali na wataalamu wa Halmashauri, pia litahusisha upokeaji wa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali (Stakeholders meeting) ili kupata taswira ya pamoja ya mwelekeo wa Jiji la Tanga.
Kikao kazi hicho kimefanyika katika moja ya ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Jiji.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.