Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia Idara ya Afya imesema inaendelea kuwahudumia wananchi, kwa kuwasogezea huduma za Afya za kibobezi karibu na Meneo yao kupitia Makambi ya matibabu ili kuwapunguzia gharama kubwa za Matibabu.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga Dkt. Charles Mkombe wakati wa hafla ya Kufunga kambi ya matibabu ya magonjwa ya Masikio, pua na Koo, iliyofanyika katika Kituo cha Afya Mikanjuni, Kata ya Mabawa.
Aidha Dkt. Mkombe amesema wagonjwa waliohudumiwa kupitia Kambi hiyo ni kutoka Jiji la Tanga, pamoja na Wilaya jirani za Handeni, Korogwe, Mkinga, Pangani na Mkoa wa Dar es Salaam huku akieleza kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu .
Kambi hiyo ambayo ilianza kwa Upimaji, Madaktari Bingwa kuwaona Wagonjwa, pamoja na kufanya upasuaji unaotajwa kuwa wenye mafanikio Makubwa.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mikanjuni Dkt. Ummykulthum Kipanga pamoja na wadau waliofanikisha zoezi hili kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga wakiwemo Taasisi ya United Help for Internationl Children (UHIC), United help for Tanzania Children-(UHTC), Nyota Foundation na Madakatari Bingwa kutoka Zanzibar Outreach Program (ZOP) na wengine wameahidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri hiyo katika kuwahudumia wananchi.
Wagonjwa waliopatiwa Huduma ya Matibabu kutokana na Kambi hiyo Wameishukuru Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na wadau kwa kuwawezesha kupata huduma hiyo kwa gharama nafuu.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.