Afisa uandikishaji wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji ametoa takwimu za awali wa zoezi zima la uandikishwaji wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na uhakiki wa taarifa huku akisema kuwa ikiwa ni siku ya mwisho wa zoezi hilo Halmashauri ya Jiji la Tanga imeweza kufikia lengo kwa kiasi kikubwa.
Mayeji amesema kuwa mpaka sasa zaidi ya watu elfu 72 wameshajiandikisha na kuhakiki taarifa zao kati ya lengo la watu elfu 75 waliopangiwa kuwaandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
"Katika Jiji la Tanga tulikadiria kuandikisha watu elfu75 na mpaka jana tarehe 28 tumeandikisha wapiga kura wapya elfu arobaini na mbili mia mbili arobaini na nne ",.Alisema Afisa uandikishaji wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Sambamba na wapiga kura wapya pia Mayeji amesema kuwa kwa upande wa waliojitokeza kuboresha taarifa zao ni jumla ya watu elfu therathini mia tatu ishirini na sita .
Mayeji amesema kuwa anaimani kuwa watu watajitokeza kurekebisha taarifa na kujiandikisha mpaka kufikia tamati ya zoezi la uandikishaji watakuwa wamefikia lengo walilopewa .
Pia Mayeji ameendelea kuwakumbusha watu kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili kuweza kupata haki ya kuchagua viongozi wanaowahitaji watakao waletea maendeleo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.