Halmashauri ya Jiji la Tanga umesaini mkataba wa Tsh.Bil 1.2 na kampuni ya M/s. M/s PROCESL EngenhariaHidraulica e Ambiental, S.A kutoka Ureno(Portugal) pamoja na Mkandarasi Mshauri ENGIDRO – Engineering Solutions, Lda Ureno( Portugal) na ENV Tanzania Ltd kwa lengo la kuandaa mpango kabambe wa Mifereji ya Maji ya Mvua na Mfumo wa Maji Taka katika maeneo yote ya jiji la Tanga, na leo ikiwa ni awamu ya kwanza ya uwasilishwaji wa mpango kabambe wa kudhibiti maji ya mvua na mafuriko.
Mhandisi Kaniki Omary amesema mpango huo umeanisha Mifereji yote ya maji ya mvua iliyopo na itakayopendekezwa kwa mujibu wa usanifu utakaofanyika (Drainage Network for the City) na pia utaainisha miradi ya kipaumbele ya muda mfupi (Miaka 5), muda wa kati na muda mrefu wa mifereji ya maji ya Mvua ambayo yatadhibiti mafuriko.
Mradi umeanza kutekelezwa kuanzia mei,2019 na utadumu kwa miezi 12, na wakati wa uandaaji wa mradi huu, viongozi na wadau wa maendeleo wa Jiji la Tanga watahusishwa katika hatua zote.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.