Halmashauri ya jiji la Tanga limeazimia kupunguza athari za mimba katika umri mdogo na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI, malengo haya yatafikiwa kufuatana na programu iliyotoa mafunzo ya masuala ya UKIMWI yaliendeshwa na wataalam wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa jiji hilo.
Kupitia programmu ya hiyo, Halmashauri ya Jiji la Tanga limefanikiwa kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi wa darasa la tano, sita na saba wapatao 1689 kwenye kata za Kirare, Mzingani na Mnyanjani kwa ajili mafunzo ya masuala ya UKIMWI, stadi za maisha na ukatili wa kijinsia.
Mratibu wa UKIMWI wa Jiji la Tanga bwana Mosses Kisibo alisema mafunzo hayo yana malengo ya kumuwesha kijana hasa mwanafunzi kupata uelewa wa masuala ya Ugonjwa wa UKIMWI na athari zake katika jamii inayomzunguka na kuchukua taadhari. Aliongeza mafunzo hayo yatawasaidia kuepukana na Mimba katika umri mdogo hasa kwa mabinti wa kike ambao wapo katika vishawishi vikubwa na kuaribiwa ndoto zao za baadae.
Kwenye program hiyo wanafunzi walipata masomo mbalimbali yakiwa na nia ya kuwapa uelewa wa masuala ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ikiwa ni pamoja na njia za maambukizi na tabia hatarishi zinazopelekea kujiingiza katika tabia hatarishi, njia za kujikinga ili kufikia ndoto zao, maana ya stadi za maisha na hatua za za stadi za maisha na faida zake kwa wanafunzi, maana ya ukatili wa kijinsia na aina za ukatili wa kijnsia na athari zake.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Kirare, wakizungumza baada ya mafunzo hayo, walishukuru kwa mafunzo maana yamewapa uelewa wa masuala ambayo kwa hakika walikuwa kwenye hatari kubwa. “Binafsi kuna vitu vingi ndio imevijua leo hii, nashukuru sana na sasa ninajitambua na naweza kuwahabarisha na wenzangu” alisema Mwasiti Ally mwanafunzi wa darasa la saba.
Kwa mijibu wa takwimu za viashiria vya UKIMWI kundi la vijana lenye umri wa kati 15-49 ndio limeathirwa zaidi kwa asilimia 6.2 na watoto miaka 0-14 ni asilimia 0.5 umri wa kundi ili wengi wamejiingiza kwenye masuala ya ngono na vitendo vya ulawiti.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.