Madiwani kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Jumatatu Desemba 30, 2024, wamefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maeneo ya ukusanyaji wa mapato, uzoaji wa takataka na utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
Madiwani hao, baada ya kuwasili katika Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, walipata mawasilisho ya miradi kutoka kwa wataalamu wa Jiji la Tanga, na baadae kutembelea Jengo la kitega uchumi lililopo kituo kikuu cha mabasi Kange (Dkt. Samia Suluhu Hassan Business Centre), kiwanda cha ufyatuaji wa tofali Gofu, Dampo la kisasa lililopo mtaa wa Mpirani, Chongoleani, kisha kufanya utalii wa ndani katika Mapango ya Amboni.
Ziara hiyo ya madiwani na Wataalamu imeongozwa na Naibu Meya wa Jiji hilo Mhe. Fadhili Chibago, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko, ambapo walipokelewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloow, pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Tanga Eng. Juma Hamsini.
Akizungumza na wageni hao, Mstahiki Meya Shiloow amesema ziara hizo zina umuhimu mkubwa katika kujifunza na kusaidia suala zima la ukusanyaji wa mapato na amewahimiza wakusanyaji wa mapato kuongeza kasi ya ukusanyaji ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Story: Salma Ramadhani
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.