Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ndg. Sipora Liana amewaongoza Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutembelea na kukagua kazi ya umaliziaji wa jengo la kitega uchumi linalojengwa katika kituo kikuu cha mabasi cha Kange Jijini Tanga.
Jengo hili lilianza kujengwa mwezi Julai 2019 kwa fedha za Serikali kuu na linatarajiwa kugharimu kiasi cha shillingi billioni 8.8 hadi kukamilika kwake. Kukamilika kwa mradi huu kutaiongezea Halmashauri uwezo wa kutoa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wake na kuwa chanzo cha mapato kwa Halmashauri.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.