Alhamisi, Oktoba 06, 2022.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Hashim Mgandilwa ameshiriki katika uzinduzi wa zoezi la uwekaji wa hereni za kieletroniki kwa ng'ombe lililofanyika katika eneo la Pingoni kata ya Maweni lenye lengo la kuitambua mifugo na kulinda mizunguuko yake.
Akizungumza na wanahabari baada ya zoezi hilo, Mhe. Mgandilwa amesema lengo ni kutoa hamasa kwa wafugaji waone umuhimu wa kuwavalisha ngombe hereni za kielektroniki ili kulinda mizunguko ya mifugo yao na kuwa na kanzi data ya mifugo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Sehemu ya Mifugo na Uvuvi Jiji la Tanga, Dkt. Paul Kisaka amesema hereni hizo zitasaidia kutambua mifugo ya ndani ya nchi na ya kutoka maeneo mengine jambo litakalo saidia kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji
Kwa upande wake Bi. Mariamu Shekue ambaye ni mfugaji wa ng'ombe wa maziwa amesema amefurahishwa na zoezi hilo kwa matumaini kuwa litasaidia kutatua tatizo kubwa la wizi wa ng'ombe ambalo ndio kilio cha wafugaji wa ng'ombe wa maziwa.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.