Halmashauri ya Jiji la Tanga, limekusidia kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana, hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Bw. Daud Mayeji akiwa kwenye Baraza Maalum la Madiwani lilifanyika kwenye ukumbi wa Jiji la Tanga. “Suala la kuwawezesha wanawake na vijana lipo kisheria na limesemwa kwenye miongozo yetu ya bajeti, sisi kama halmashauri hatuna budi kutekeleza hilo”
Kama ilivyoelekezwa kwenye miongozo, halmashauri ilishawapatia fedha za mikopo baadhi ya vikundi. Pamoja na kutoa fedha hizo, lakini kumekuwa na changamoto nyingi sana kwenye kufanya marejesho ya mikopo hiyo. “Kwa sasa halmashauri inapitia vikundi vyote vilivyopewa mikopo na kuendelea kufanya ufuatiliaji wa marejesho ili fedha hiyo iendelee kukopesha wengine”alisema Mkurugenzi.
Halmashauri inaendelea na taratibu za kutambua vikundi na kuvisajili halmashauri ambapo awali vikundi vingi vilikuwa vimejisali kwa Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA). Kitendo hiki ni kinyume na utaratibu wa usajali wa vikundi vilivyokusudiwa kupata fedha hizi. Muongozo wa kukopesha fedha hizi kwa kikundi unataka kikundi lazima kimesajiliwa kwenye halmashauri husika ndipo kipate mkopo.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii, Bi Flora Shija amesema halmashauri inaendelea kutoa elimu ya namna ya kufanya usajili wa vikundi kwenye ngazi ya halmashauri na kuwapa namna bora ya kutumia mikopo hiyo ili kuleta tija ya maendeleo na kuweza kurejesha mikopo. “Hadi sasa tunaendelea kutoa elimu kwa vikundi vya wanawake, vijana, walemavu na wengineo, na tarehe 9 mwezi huu tutakuwa na mafunzo ya usajili wa vikundi vya kiuchumi wa kijamii kwenye ukumbi wa Tangamano hapa jijini Tanga” alisema afisa huyo alipokuwa naongea na mwandishi wa habari hii.
Kwa upande wao, waheshimiwa madiwani wa jiji hilo wameonesha kufurahia mpango wa vikundi kupewa vifaa na vitendea kazi badala ya kupewa fedha maana kumekuwa na mtindo wa wanakikundi kugawana fedha na kushindwa kufanya shughuli kama kikundi, hali hii inapelekea kushindwa kufanya marejesho kama utaratibu wa mikopo unavyotaka.
Kwa mujibu wa sheria na miongozo ya bajeti, Halmashauri zinatakiwa kutoa asilimia 10 ya bajeti ya mapato yake ya ndani 5% kwa wanawake na 5% kwa vijana (vijana wa kike na wa kiume wa miaka kati ya 15 na 35) kiwango hiki hutolewa kama mkopo wenye masharti nafuu kwa makundi hayo ili kuweza kufanya shughuli za kimaendeleo na kisha kurejesha mkopo huo kwa faida ya asilimia 10 kwa mwaka. Kwa mwaka wa fedha 2017/18, halmashauri ya Jiji la tanga limetenga jumla ya Tsh. Milioni 640 kwa ajili ya vijana na wanawake.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.