Kamati ya lishe ya Halmashauri ya Jiji la Tanga iliyokutana Oktoba 28, 2022, imepokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 iliyowasilishwa na Afisa Lishe wa Jiji, Sakina Mustafa, ikionyesha kupata mafanikio makubwa katika mpango na utekelezaji wa bajeti, pamoja na kuwajengea uwezo watumishi 24 juu ya matibabu ya utapiamlo.
Shughuli za lishe zinasimamiwa na Kitengo cha Lishe chini ya Idara ya Afya, na kushirikiana na Idara, Vitengo na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha afya na hali ya lishe ya makundi maalum zinaboreshwa.
Taarifa zinaonyesha kuwa, katika robo iliyomalizika, Halmashauri yetu imekuwa ya 36 kati ya Halmashauri 184 nchini katika utekelezaji wa masuala ya lishe.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.