Leo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe ametembelea kiwanja kinachotarajiwa kujenga kituo cha michezo kata ya mnyanjani jijini tanga.
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo imeomba Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) zaidi ya Bil.4 ili kujenga Kituo hicho ambacho kitakuwa na viwanja vinne na Hosteli za wanafunzi wana michezo watakachokuwa wanakaa kambini katika kipindi chote cha lafunzo.
Waziri Mwakyembe pia ameahidi Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuanza haraka mchakato wa kufanikisha “Tanga inasifika vizuri sana kwa kutoa wana michezo mahiri sana hivyo Serikali imeamua kuanzisha kituo cha Michezo eneo hili la mnyanjani hapa Tanga na Fifa wameshatenga Bil.4, sasa kuna haja ya TFF kuanza mara moja ujenzi wa kituo hicho na wizara itahakikisha fedha hizo zinatumika zilivyokusudiwa” amesema Waziri Mwakyembe.
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF, Khalid Abdallah amemweleza Waziri kuwa kwa mujibu wa ramani vitajengwa viwanja vine ndani ya eneo hilo la kituo cha kufundishia soka kwa vijana na majengo mbalimbali yanayohusiana na soka.
Mkurugenzi wa jiji la Tanga Daudi Mayeji amesema eneo hilo lina ukubwa wa heka 7.6 na kwamba fidia zimeshatolewa kwa nyumba zilizo ndani ya kituo hicho tarajiwa ndiyo maana eneo lipo wazi.
Aidha katika ziara hiyo Waziri Mwakyembe pia ametembelea uwanja wa mpira wa mkwakwani kuona uwanja ulivyo na kushauri namna ya kuboresha kiwanja hiko ili kiweze kujiingizia mapato, kiwanja cha Mkwakwani ni kiwanja kikubwa jiji la Tanga ambapo ligi kuu za Tanania au mechi za kirafiki pia uchezewa hapo.
Pia Mhe.Waziri wa Habari amefungua mafunzo ya namna ya kutengeneza vipindi vya Umma kwa Washitiri ambao ni maafisa Habari kutoka Taasisi mbalimbali za Umma nchini Tanzania “Tuhabarishe wananchi azma yetu kufikia malengo mwaka 2025 ya Maendeleo Kiuchumi,Kijamii na sera ya habari inasisitiza uwepo wa Mawasiliano bora kwa kuzingatia maadili ya taaluma, ni wajibu mkubwa na wenye dhamana” Amesema Waziri Mwakyembe.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.