Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mhandisi Juma Hamsini, leo Jumatatu Desemba 23, 2024, amefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Sekondari katika Kata ya Majengo (ilipokuwa Shule ya Msingi Chuma), na kiwanda cha ufyatuaji tofali cha Halmashauri ya Jiji kilichopo eneo la Gofu viwandani.
Katika eneo la kiwanda cha matofali, Mhandisi Hamsini, ambaye aliongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Silikanti, inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga, ambayo ndiyo inayokiendesha kiwanda hicho, Wakili Idrisa Mbondera, amesikiliza changamoto za uzalishaji wa tofali na kutoa maelekezo ya kufanyiwa kazi ili kuhakikisha kiwanda kinafanya kazi katika uwezo wake, ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa matengenezo ya moja ya mashine ambayo kwa sasa imesimama uzalishaji kwa matatizo ya kiufundi.
Na katika hatua nyingine, Mkurugenzi Hamsini amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia yenye lengo la kuboresha tasnia ya michezo katika Jiji la Tanga.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ndani ya uwanja wa Mkwakwani, Viongozi hao wamejadili namna ya kuuboresha uwanja wa Michezo wa Mkwakwani na ujenzi wa Zahanati katika Kituo cha Michezo cha Mnyanjani.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.