Wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wametakiwa kutoa ushirikiano kwa wadau wanaopinga masuala ya ukatili kwa watoto ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo katika Halmashauri hiyo.
Hayo yamesemwa na Afisa elimu ,kilimo na mazingira Enedy Mwinzava wa Halmashauri ya Jiji la Tanga katika kikao kilichowakutanisha Maafisa maendeleo ya Jamii ,Walimu ,Kamati za wazazi pamoja na Wanafunzi kutoka shule ya msingi Mabawa ,Shaban Robert,pamoja na Majengo ambapo amesema Jiji hilo linaongoza kwa matukio ya ulawiti kwa watoto.
“Tafiti zimefanyika na Tanga tumeonekana kushika nafasi ya kwanza katika ukatili kwa watoto wetu wanafanyiwa vitendo vya ngono na wanaofanya hivyo ni jamii yetu inayotuzungua hivyo Jiji imeamua kuandaa kampeni hii ya kupita katika shule zetu na kukutana na Walimu ,Kamati za wazazi pamoja na Wanafunzi na kutoa elimu kwani watoto wetu wanateketea”,.Alisema Enedy Mwinzava Afisa elimu Kilimo na Mazingira
Pia Enedy ameongeza kuwa kuvunjika kwa ndoa ,umasikini , wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni pamoja na uhuru kwa watoto ndio sababu kubwa inayosababisha vitendo vya ulawiti kwa watoto kuongezeka .
Kwa upande wake Loveness Robert ambae ni mwalimu wa Shule ya Msingi Shabani Robert amesema wazazi pamoja na jamii wanapaswa kushirikiana ili kuhakikisha wanawasaidia watoto wao .
“Ifike mahali sisi wazazi na jamii tutambue majukumu yetu kwa watoto wetu kwasababu endapo mzazi utakuwa makini na mtoto wako haya mambo ya ulawiti kwa watoto wetu hayatakuwepo kwa sababu tunawaacha watoto wetu mpaka saa 9 za usiku wakiwa kwenye vigodoro harafu tunakuja kulalamikia serikali lakini tukiwa makini nao haya yote hayatajitokeza “,. Alisema Loveness Robert mwalimu wa shule ya msingi Shabani Robert
Licha ya changamoto hizi Halmashauri kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo ya Jamii wameandaa mpango kabambe kwaajili ya kudhibiti jambo hili na kauli mbiu ya kampeni hii ni MIMI NI MTOTO NAJITAMBUA SISHABIKII MAPENZI.
Wanafunzi kutoka shule ya msingi Mabawa,Shabani robert pamoja na Majengo wakiwa wamenyoosha vidole kwa ajili ya kujibu swali waliloulizwa
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.