Desemba 16, 2023.
Na; Mussa Labani, Tanga.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Umoja wa Amani Kwanza, imefanya hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kudumisha, kusimamia na kutunza misingi ya amani na usalama kwa taifa. Hafla hiyo iliyofanyika Jijini Tanga, ilihudhuriwa na viongozi na wawakilishi kutoka sekta mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ndg. Said Majaliwa ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuandaa hafla hiyo na kuahidi kuwapa ushirikiano kwa namna yoyote, na kuahidi kuyafikisha maombi aliyopewa, kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba.
Majaliwa amesema tukio hilo ni ishara ya Taasisi hiyo kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kudumisha amani na usalama ili kuweka mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo. Amesema nchi ikikosa amani, ni vigumu kufanya kazi za maendeleo na hata wawekezaji hawawezi kuwekeza katika nchi ambayo haina amani.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.