Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Japhari Kubecha, leo Desemba 20, 2024 amefanya ziara katika kiwanda cha matofali cha Halmashauri ya Jiji la Tanga, kilichopo eneo la Gofu viwandani.
Katika ziara hiyo Mhe kubecha ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanafyatua tofali 4500 kwa siku, badala 1200 zinazofyatuliwa kwa sasa, na kuahidi kurudi kukagaua baada ya siku 4.
Aidha Mhe Kubecha amemataka aliyekuwa Meneja wa kiwanda hicho hadi kufikia Desemba 23, 2024 awe amelipa gharama ya mifuko 24 ya saruji iliyoharibika kiwandani hapo.
Story: Rashidi Said
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.