Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Japhari Kubecha, leo jumanne, Januari 14, 2025 amefanya ziara katika kata za Nguvumali na Mwanzange kwa lengo la kukagua hali ya usafi katika kata hizo.
Katika ziara hiyo Mhe. Kubecha amemuagiza Afisa Biashara anaye simamia soko la Mgandini na Mtendaji Kata wa Kata ya Mwanzange, kuwatoza faini wauza nyama wote wasiofuata utaratibu uliowekwa ikiwemo kuvalia mavazi maalumu ya kufanyia biashara hiyo na pia amewataka wauza Samaki kutofanya biashara ya Samaki mpaka watakapo safisha meza zao na maeneo wanayofanyia biashara.
Aidha Mhe. Kubecha ametoa muda wa mwezi mmoja kuhakikisha soko hilo linawekewa chombo cha kuhifadhia taka taka {skip bucket}
Na katika hatua nyingine, Kubecha ametoa siku mbili kwa kitengo cha udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira Jiji la Tanga kuhakikisha mitaro ya maji ya mvua iliyopo eneo la Nguvumali Jeshini inasafishwa ili kuweka eneo hilo katika hali ya usafi.
Story: Rashidi Said
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.