Shule sita za Msingi katika Jiji la Tanga zitanufaika na mradi wa uboreshaji upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) kwa mwaka wa fedha 2022/2023, ambapo kiasi cha zaidi ya shilling million 940 zitatumika kwa ujenzi wa shule mpya moja, vyumba vya madarasa 12, Madarasa 2 ya elimu ya awali na matundu 15 ya vyoo.
Katika kufanikisha utekelezaji wa miradi hii, timu ya usimamizi wa utekeleaji wa mradi ngazi ya Halmashauri, chini ya Mratibu wa Mradi, Mwl. Leen Chamba, imeendelea kukutana na jamii inayozunguuka mradi kwa lengo la kuwataarifu mapokezi ya fedha za mradi, na kuielimisha jamii juu ya faida na hatua za utekelezaji wa mradi, kwa kuzingatia miradi ya BOOST inaelekeza ushirikishwaji wa jamii kwa kila hatua ya ujenzi.
Shule sita za Msingi za Jiji la Tanga zitakazo nufaika na mradi kwa mwaka huu wa fedha ni pamoja na ujenzi wa shule mpya Jaje, Madarasa mawili ya elimu ya awali Mapojoni, vyumba vitatu kwa kila shule za Bombo, Mabawa, Mapambano na Msala. Ambapo ujenzi wa majengo hayo utajumlisha na ununuzi wa madawati, meza na kiti cha Mwalimu kwa kila darasa.
Wakati Jiji la Tanga likiwa limepokea shilling million 940,900,000.00, jumla ya fedha ya BOOST kwa mwaka huu wa fedha iliyotolewa kwa Mkoa wa Tanga ni shilling Billion 11,422,000,000.00 ambapo shule mpya za Msingi 15 zitajengwa, sambamba na vyumba vya madarasa 140 pamoja na miundombinu mingine.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.