Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi.Pili Hassan Mnyema amezindua rasmi Mradi wa TIMCI (Tools for Integrated Management of Childhood Illiness) katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.
TIMCI imelenga Kuboresha Upatikanaji wa Vifaa vinavyosaidia kugundua magonjwa makali kwa Watoto chini ya Miaka Mitano.
“Mradi huu ukalenge kupunguza vifo vya Watoto, Mkoa wa Tanga una vifo vya watoto waliofia tumboni 64, watoto waliofariki mara baada ya kuzaliwa 65 na Vichanga wa siku 0-28 wakiwa 53 kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa hai katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2021, kipaumbele cha Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Sita Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa Wananchi wake imetunga sera y matibabu bure kwa watoto chini ya miaka mitano, hivyo basi ji wajibu wetu sote kuzingatia utekelezaji wa sera hii kwaajili ya kuboresha afya za watoto wetu na kuzuia vifo ambavyo vingeweza kuepukika”. Alisema Bi.Pili Hassan Mnyema Katibu Tawala akizindua mradi huo.
Mradi huu utawezesha watoa huduma za Afya kutoa huduma stahiki za Uchunguzi na Utambuzi wa magonjwa ya watoto chini ya Miaka mitano kwa kutumia vifaa tiba vya kupima Oksjeni mwilini (POX) na vifaa saidizi vya maamuzi vya kielectroniki (eCDSA).
Halmashauri ya Jiji la Tanga ni moja kati ya Wanufaika wa 3 katika wilaya 3 zilizoteuliwa ikiwa pamoja na Sengerema na Kaliua kwa Nchi ya Tanzania, takwimu za kutoka kwenye mfumo wa taarifa za afya zinaonesha kuwa kipindi cha Januari mpaka Machi 2021, kwa jiji la Tanga watoto waliofia tumboni 31, watoto waliofariki mara baada ya kuzaliwa 38, vichanga kuanzia siku 0-28 wakiwa 34 na chini ya Miaka mitano 14 kati ya Watoto 1,000 waliozaliwa hai.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.