Baraza la Madiwani jijini Tanga limewakufukuza watumishi 11 na kupunguza mshahara mtumishi mmoja kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu ikiwemo utoro kazini na matumizi mabaya ya fedha za wananchi wa jiji.
Akitoa taarifa hiyo Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Mhe.Seleboss Mustafa amesema kufukuzwa kazi kwa watumishi hawa kumetokana na kuzorotesha kazi na kuchelewesha maendeleo kwa wananchi, amewataja watumishi hao mtendaji wa mtaa Jamhuri B kata ya Ngamiani,Joachim Mabula Tabibu daraja la II, Mtendaji wa mtaa wa old Nguvumali kata ya Nguvumali, Mtendaji wa mtaa Mahako Mbugani, Mtumishi wa Zahanati Kichangani, Mtendaji wa mtaa wa Mbezi B kata ya Makorora, Mtendaji mtaa Tikila,Magumila,Shabani Juma mhasibu Ngamiani, Muuguzi daraja la II Ngamiani na Aggy Mohamed amepunguziwa mshahara ambaye ni mtendaji mtaa wa kwanjekaNyota.
Mstahiki Meya katika Mkutano huo amesema Baraza halitamuonea mtendaji yoyote wala halitashindwa kumchukulia hatua mtumishi yoyote wa Halmashauri ambaye yupo ndani ya mamlaka ya baraza ya kinidhamu isipokuwa Mkurugenzi tu lakini wakuu wa idara, watendaji wa kata na mtaa wapo ndani ya mamlaka yao ya kinidhamu, lengo ni kufanya halmashauri iwe na nidhamu alisisitiza Mstahiki Meya.
Aidha katika kuhitimisha Mkutano huo, Mstahiki Meya wa jiji la Tanga kwa niaba ya wananchi wa Tanga kwa pamoja wamempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mhe.John Joseph Pombe Magufuli kwa kutoa Bil.17 kwa jiji la Tanga ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususani kwenye sekta ya elimu, afya na uchumi.
Katika fedha hizo Bil.3 imeelekezwa kujenga vituo vya afya 6, Bil.1.5 kujenga Hospital ya wilaya ya Tanga, Bil.8.3 hii ikiwa imeelekezwa kujenga kitenga uchumi katika stendi ya mabasi Kange ambacho kitakuwa na huduma zote muhimu kwa jamii.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.