Na Kelvin Beda, Tanga.
Jumla ya wanafunzi 6745 ambao ni sawa na Asilimia 85 wameripoti shule kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza huku wanafunzi zaidi ya 1250 sawa na asilimia 15.7 hawajaripoti mpaka Sasa katika Jiji la Tanga.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa wakati wa ziara yake ya ufuatiliaji wa maendeleo ya zoezi la uandikishaji wa Wanafunzi kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za Sekondari Jijini hapa.
Amesema kuwa mpaka sasa shule ambazo zipo katika kata za mjini zimekuwa hazifanyi vizuri Kwa kuwa na uandikishaji wa chini ya asilimia 60 mpaka Sasa.
"Natoa wiki Moja idara ya elimu msingi na Sekondari sambamba na watendaji wa mitaa kuja na taarifa za wapi watoto wengine ambao mpaka Sasa wameshindwa kuripoti shule na sababu zao" Amesema DC Mgandilwa.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya amepiga marufuku michango ya aina yoyote ambayo inachangwa katika shule bila ya kufuata utaratibu wa kibali kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa wilaya.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.