Uwepo wa Baadhi ya Madereva wa vyombo vya moto wasiofuata Sheria za Barabarani imetajwa kuwa chanzo cha Ajali ambazo zimekuwa zikitokea katika maeneo yanayozunguka Shule.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend ikifadhiriwa na Fondation Botnar imeendelea kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa Madereva wa vyombo mbalimbali vya Moto katika Jiji la Tanga kwa kutumia Wanafunzi wa Shule za Msingi.
Ramadhani Nyanza ni Mratibu wa Miradi Shirika la Amend ambao ni Wadau wa Usalama Barabarani amesema kwa kutumia Mahakama ya Kifani ya Watoto, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani wamefanikiwa kutoa Elimu kwa Madereva kuhusu Makosa mbalimbali ya Barabarani..
Inspekta George Elihaki ni Mkaguzi wa Magari na Mtahini wa Madereva, amepongeza Taasisi hiyo kwa kuendelea kutoa Elimu kwa Madereva hao na kuitaka jamii kuendelea kutoa Ushirikiano kwa Jeshi hilo katika kutokomeza Ajali za Barabarani.
Athumani Babu ni Diwani wa Kata ya Mabawa,akaliomba Shirika hilo kutanua Wingo wa utoaji wa Elimu hiyo ikiwemo kwa Madereva wa Pikipiki marufu kama Bodaboda Pamoja na Waenda kwa Miguu.
Madereva waliopatiwa Elimu ya Makosa ya Usalama Barabarani wamesema Elimu hiyo ni muhimu kwao huku wakiwashauri Madereva wenzao kuzingatia Sheria za Kazi zao.
Wanafunzi walioshiriki katika Mahakama ya Watoto katika utoaji wa Elimu,wamesema watakuwa Mabalozi wazuri wa Usalama Barabarani.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.