Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, leo alhamisi, Januari 23, 2025, imefanya kikao chake cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025, kilichoongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Dkt. Stephen Mwandambo, ambacho kimepokea na kujadili shughuli za afua za lishe kwa kipindi hicho.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2024, Afisa Lishe wa Jiji, Rehema Kirungi, amesema jumla ya wajawazito 10,888 sawa na asilimia 100 ya waliohudhuria kliniki ya baba, mama na mtoto, walipewa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu pamoja na elimu ya mlo kamili ili kuboresha hali ya afya na lishe katika kipindi cha ujauzito.
Kirungi amesema kwa sasa shule zote za Msingi na Sekondari katika Jiji la Tanga, zinatoa angalau mlo mmoja kwa siku, huku watoto 42,393 wamefikiwa katika zoezi la utowaji wa nyongeza ya matone ya Vitamini 'A' pamoja na dawa za minyoo.
Shughuli za lishe zinasimamiwa na kuratibiwa katika Idara ya Afya na utekelezaji wake unahusisha Idara mtambuka, pamoja na wadau mbalimbali wanao jishughulisha na afua za lishe.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.