• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

Majukumu Maalumu ya Kamati ya fedha na uongozi

(i)        Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato  

(ii)        Kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti na mpango wa maendeleo kwenye Halmashauri ili kuidhinishwa na Halmashauri.

(iii)       Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta                   madeni, na kuomba vibali maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.    

(iv)      Kufikiria na, pale inapowezekana, kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu Sheria Ndogo na utendaji katika                  ngazi za chini za Halmashauri.

(v)       Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili  matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisio                           yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri.

(vi)      Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye                        Halmashauri.

(vii)     Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri.

(viii)     Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa Sheria ya fedha za Serikali za                   Mitaa, sura ya 290.

(ix)      Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na              maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.

(x)       kusimamia na kuthibiti matumizi ya fedha za Halmashauri, kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Waziri na taratibu nyingine                zitakazowekwa na Halmashauri.

(xi)      Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususan kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara              yanayohusu thamani ya fedha ambapo kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vita hutumika.

(xii)      Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali vinavyotolewa na Halmashauri.

(xiii)     Kufikiria mapendekezo ya Bajeti na mipango ya Maendeleo ya kila Kamati ya kudumu na kuiwasilisha kwenye Halmashauri ili                 kupata idhini.

(xiv)    Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatu stahiki ya kuchukua kuondoa mapungufu              katika mapato au ziada matumizi.

((xv)   Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye Halmashauri ili kupata                idhini.

(xvi)    Kupokea mahesabu ya mwaka ya Halmashauri na kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa                Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

(xvii)   Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia mpango wa Bajeti uliopitishwa na Halmashauri.

(xviii)   Kupitia taarifa ya kila robo mwaka kuhusu manunuzi iliyowasilishwa na Afisa Masuuli;

(xix)    Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa.

(xx)     Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuzi  au ukaguzi wa huduma au vifaa vilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi,                          itafanyika hivyo endapo itadhihirika kwamba, maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma hayaridhishi.

(xxi)    Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu wa Sheria husika.

(xxii)    Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayowasilishwa kwenye Kamati na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua.

(xxiii)   Kupendekeza njia na taratibu za kuondosha vifaa chakavu.  Uondoshaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au                    kuviharibu

(xxiv)  Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo mwaka;

(xxv)   Kupendekeza kwa Halmashauri hatua za kuchukua kuhusu kufuta madeni ya Halmashauri

(xxvi)  Kushughulikia sera kuhusu kukopa na uwekezaji

(xxvii) Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano wa Halmashauri nyingine.

(xxviii) Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya mapato ya vijiji na miji midogo kwa mujibu wa sheira

(xxix)  Kuteua wakaguzi wa fedha/mali za Serikali za vijiji kwa mujibu wa Sheria sura ya 290.

(xxx)   Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kuhusu mambo yote yanayohusu masuala ya ajira na kinidhamu ya                  wafanyakazi na watumishi.

(xxxxi) Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.

(xxxii)  Kupokea na kutoa uamuzi juu mapendekezo ya watumishi wanaokwenda masomoni

(xxxiii) Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri,            matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.

(xxxiv)  Kupitisha mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika               ya utumishi.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.