USIJENGE KIHOLELA, TAMBUA MAMBO HAYA MUHIMU KUHUSU KIBALI CHA UJENZI
1. KIBALI CHA UJENZI
Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo Mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya:-
(i) Kutuma maombi kwa mamlaka ya mji
(ii) Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika
(iii) Kupata kibali kwa maandishi kinachoitwa “Kibali Cha ujenzi”
2. KIBALI CHA AWALI (Planning consent)
Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outland plan) kwa utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho.
Faida:
• Kuokoa muda na gharama iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
•Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.
3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI
Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe ifuatavyo:-
• Seti tatu za michoro ya jengo (Archectural drawing)
• Seti mbili za michoro ya vyuma/mihimili (structural drawings) kwa michoro ya ghorofa
4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI
Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-
5. VIAMBATANISHO
Fomu za maombi zilizojazwa kwa usahihi
Hati ya mmiliki wa kiwanja au barua ya toleo
Kumbumbuku nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo, makabidhiano n.k
Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo
Mabadiliko ya matumizi ya ardhi
6. HATUA ZINAZOFUATWA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA KIBALI
Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:-
7. TARATIBU ZA KUFUATA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
Kwa mujibu wa sheria ya ujenzi mijini ujenzi wowote ambao
umepata kibali unapaswa kukaguliwa kwa kila hatua ya ujenzi. Baada ya kupata kibali cha ujenzi mambo yafuatayo yanapaswa kufanyika:-
1. Kutoa notisi ya masaa 48 kabla ya kuanza ujenzi. Fomu ya notisi hii utapatiwa unapokabidhiwa kibali cha ujenzi
2. Kujaza fomu ya ukaguzi na kuwasilisha kwenye ofisi ya ujenzi ili hatua hiyo ya ujenzi unayotaka kufanya ikaguliwe
3. Utapatiwa “Certificate of Occupation” baada ya ujenzi wako kukamilika iwapo tu hatua muhimu za ujenzi zimekaguliwa
8. FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA IKIWA NA KIBALI CHA UJENZI
Kuishi kwenye nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama
Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji uliopangwa
Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali ikiwa pamoja na kushitakiwa mahakamani, kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.
Hayo ndio Mambo muhimu ya kuyafahamu kuhusu 'Kibali cha Ujenzi' (Building Permit),
Epuka usumbufu fata sheria!.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.