UWEKEZAJI WA MAENEO YA VIWANDA (INDUSTRIAL PARKS)
Pongwe Industrial Parks:
Eneo hili lina ukubwa wa ekari 131 lina jumla ya viwanja 101 katika ya hivyo 98 ni eneo la viwanda, 2 maeneo ya vituo vya mafuta na 1 eneo kwa ajili ya wafanyabiashara (vijana na wanawake)
Kazi ya upimaji wa viwanja husika imefanywa na Chuo cha Ardhi Morogoro ambayo imegharimu Tshs 298,894,599 kwa viwanja 4,707.
Halmashauri inatarajia uwekezaji mkubwa kwenye eneo hili la viwanda kwa kujumuisha viwanda vya aina mbalimbali kama viwanda vya uzalishaji wa chakula, viwanda vya vifaa vya kielektroniki, viwanda vya nguo, uzalishaji wa vifaa vya ofisini na uunganishaji na utengenezaji wa magari.
Upatikanaji wa viwanja ni pamoja na kupangisha eneo kwa kulipa kodi kwa Halmashauri, kuingia ubia na Halmashauri au kununua kiwanja. Sambamba na eneo hilo la viwanda Halmashauri imepima eneo lingine lenye ukubwa wa ekari 129 kwa ajili kutoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi watakaoishi kwenye eneo jirani na viwanda 29 na maeneo ya umma 11 ambapio ikadiriwa wananchi 3,000 wataishi kwenye eneo hilo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.