KIOMONI AND MABOKWENI INDUSTRIAL PARKS:
Halmashauri iliingia makubaliano ya kiungwana (Memorandum Of Understanding – MOU) na mmiliki wa shamba la Amboni “COALTAIL LIMITED” ili kuendeleza shamba la Amboni. Katika makubaliano hayo Halmashauri tayari imeanza kutekeleza makubaliano hayo kwa kuandaa ramani za Mipango Miji katika maeneo ya Mabokweni, Mikocheni na Pande ambapo jumla ya viwanja 4000 vinategemewa kupatikana na kupimwa ili hatimaye kumilikishwa kwa watu mbalimbali. Mpaka sasa hatua iliyofikiwa ni urejeshaji wa hati miliki ya awali za mashamba hayo ambapo hati hizo zimeshapelekwa kwa Kamishna Msaidizi kwa hatua hizo za mwisho.
Aidha, kutokana na Makubaliano hayo ya Kiungwana (MOU) kati ya Halmashauri na Coaltel Enterprises ambapo Halmashauri ilipewa eneo lenye ukubwa wa ekari takribani 5000, Halmashauri inakamilisha upimaji kwenye maeneo miongoni mwa yaliyotolewa na Coaltel Enterprises ambayo yataitwa Kiomoni Industrial Park yenye viwanja 112 na Mabokweni Indusrial Park yenye viwanja 117 na upimaji wake unakadiriwa kukamilika ifikapo mwishoni mwanzoni mwa Machi 2018.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.