Jiji lina eneo la hekta 60,000 ambapo hekta 35,000 kati ya hizo zinafaa kwa kilimo. Kati ya hekta hizo zinazofaa kwa kilimo ni hekta 20,000 ndizo zinazotumika kikamilifu kwa kilimo. Eneo lililobaki linatumika kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo ikiwemo ufugaji na viwanda. Kati ya idadi ya watu waliopo katika Halmashauri ya Jiji ( 273,332) ni wakazi 52,205 ndiyo wanaoishi maeneo ya nje ya mji ambapo familia 5,600 (watu 25,000) ndizo zinazojishughulisha kikamilifu na shughuli za kilimo.
Mazao ya kilimo ni pamoja na muhogo, korosho, Nazi, katani, Bustani za mboga na matunda na mengineyo
MAFANIKO YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA KILIMO NA USHIRIKA
Kusimamia usambazaji wa pembejeo za korosho kiasi cha lita 224 katika kata za Chongoleani, Kiomoni, Kirare, Maweni, Mabokweni, na Pongwe.
Kushiriki maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini
Kuongezeka kwa eneo lililimwa na kupandwa korosho kutoka tani 64 hadi kufikia tani 100 mwaka huu
Kutoa elimu kuhusu kilimo cha umwagiliaji kwa kikundi cha vijana cha Kiomoni cha Mwamko
Vyama 74 vilivyoandikishwa kisheria zikiwemo saccos 51 na vyama vingine 23
Vyama 12 vimeitisha uongozi mpya na tayari vimepata viongozi wapya kwa mujibu wa sheria na kanuni za Ushirika
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.