HATUA ZA KUFUATA
1. SAJILIWA KWENYE MFUMO
Usajili wa kwenye mfumo unafanywa na Afisa TEHAMA wa Halmashauri uliyopo (kama muombaji ni mtumishi wa Halmashauri). Ili usajaliwe yafuatayo yanahitajika:
Afisa TEHAMA atakusajili na kukufundisha namna ya kujaza fomu kwenye mtandao.
2. HUISHA AKAUNTI YAKO YA MFUMO
Baada ya kusajiliwa kwenye mfumo, utapokea ujumbe kwenye barua pepe yako (kupitia anuani uliyosajaliwa nayo hapo awali kwenye hatua ya kwanza)
Ujumbe utakupa maelekezo ya namna ya kuingia kwenye mfumo na utakutaka kubadili neno la siri/nywila (password), kisha utaweza kuingia kwenye mfumo na kuanza kufanya maombi ya kibali cha kusafiri nje ya nchi.
MUHIMU: Nywila (password) lazima iwe na sifa neno lenye urefu wa characters nane ambapo ndani yake kuwe na mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo, namba na “special characters - !@$%#” (mfano: Mtanzania123!)
3. INGIA KWENYE MFUMO
Ukifanikiwa kuingia kwenye mfumo, unatakiwa kubonyeza/kuingia kwenye aneo la “kibali cha safari”. Ili ukamilishe eneo hili, mahitaji yafuatayo lazima yatimizwe;
NOTE:
1: Kama safari ni binafsi kwa matembezi/mapumziko, lazima uwe na barua ya likizo
2: Kama safari ni matibabu ni lazima uwe na vielelezo vinaelezea Ushauri wa Kitabibu na Rufaa ya Matibabu
3: Kama safari ya ni mafunzo ya muda mrefu ni lazima uwe na;
Barua ya Udahili
Barua ya Udhamini wa Masomo
Barua ya Mwaliko
MUHIMU:
Nyaraka zote hizi ziwe zimefanyiwa scanning kwenye format ya PDF
4. KUJAZA FOMU
Mfumo unakuelekeza namna ya kukamilisha kujaza fomu mpaka mwisho. Ukiwa na nyaraka (documents) zilizoanishwa hapo mwanzo, zoezi la kujaza fomu linakuwa fupi. (Melekezo ya jinsi ya kujaza fomu yanatolewa na Afisa TEHAMA aliyekusajili kwenye mfumo)
KUMBUKA: zoezi la kujaza fomu linafanyika kuanzia hatua ya mwanzo hadi ya mwisho kwa wakati mmoja. Maana yake ni kwamba ili uanze kujaza fomu ni lazima uwe na nyaraka zilizotajwa hapo mwanzo.
Mara baada ya kukamilisha ujazaji wa fomu kikamilifu, utawasilisha fomu yako kwa njia hii ya mtandao kwa kubonyeza neno WASILISHA.
Maombi yako yatakuwa yametumwa kwenye mamlaka husika na kufanyiwa kazi (kwa ngazi ya Halmashauri maombi yanatumwa TAMISEMI). Mrejesho wa kibali chako utayapa kwa njia mtandao kama ulivyofanya maombi ya kibali.
5: NAMNA YA KUPATA MREJESHO WA MAOMBI
Mrejesho wa maombi unapatikana kwa kuingia kwenye mfumo (kama ulivyoingia wakati wa kuomba kibali), na baada ya kufanikiwa kuingiwa kwenye mfumo, bonyeza/ingia kwenye mrejesho wa safari ili kupata mrejesho. Kipindi cha kupata mrejesho baada ya kuomba kibali inategemea na mamlaka inayohusika na kupitisha vibali.
Kibali kikiwa kipo tayari, unaweza kuprint.
Kuingia kwenye mfumo, bonyeza hapa
kwa maelekezo zaidi tafadhali wasiliana na afisa TEHAMA, au fika ofisi ya kitengo cha TEHAMA - JENGO KUU LA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA, CHUMBA NA. 18
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.