• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

Tanga jiji Kinara wa kutoa mikopo asilimia 10%

Imewekwa: September 7th, 2019

Katika kutekeleza agizo la Serikali la kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Walemavu mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela amekabidhi pikipiki 70 kwa vijana wanaounda kikundi cha Tanga One Youth  Group (TOYG).

Akikabidhi pikipiki hizo  zenye thamani ya shilingi Mil.182, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela amesema amefurahishwa  kuona Tanga jiji inaendelea kuwa kinara kwa  utoaji  mikopo kwa kata zote 11 alizotembelea kwa vijana ,wanawake na walemavu ambao wamepewa mikopo .

“Ninafuraha kuona Tanga Jiji imeendelea kuwa kinara kwa utoaji wa mikopo kwa kata za Halmashauri  zote 11 za Mkoa wa Tanga  na leo tumeshuhudia vijana hawa wamekabidhiwa pikipiki hizi na kwa kila kata mmetoa kwa wanawake ,vijana na walemavu”.Amesema Mhe Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Tanga. 

Ameongeza kuwa mikopo hiyo haina riba hivyo watarudisha pesa zilezile  walizokopa  na  amewataka waliochukua mikopo kuitumia vizuri ili waweze kuirejesha na wengine kukopa.

Pia amesema amefarijika kuona Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani  ametoa  mafunzo  kwa vijana hao kabla hawajakabidhiwa pikipiki hizo hivyo hategemei tena kusikia kesi zozote kama kipindi cha nyuma .

Akisoma taarifa Afisa Maendeleo wa Jiji Bi .Dorah Ntumbo amesema kikundi hicho kimesajiliwa  Aprili 30 na kupewa namba za usajili Tcc/Kkd/2019/067, kikundi hiki  kinajishugulisha na uendeshaji wa pikipiki  za usafirishaji wa  abiria.

“Mhe Mkuu wa Mkoa ili kufanikisha malengo ya kikundi hiki Halmashauri ya Jiji la Tanga imetoa mkopo wa jumla ya Tshs Mil. 182  kwaajili ya ununuzi wa pikipiki 70 kwa ajili ya vijana na kwa kushirikiana na kamanda wa usalama barabarani vijana hawa wamepewa mafunzo ya usalama barabarani Ujasiriamali pamoja  na Ofisi  ili waweze kufanya kazi”.Alisoma Afisa Maendeleo ya Jiji Bi Dorah Ntumbo 

Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga Ndg Solomoni  Mwangamilo amesema wameamua kuwapa mafunzo hayo ili waweze kuwa watiifu katika sheria na wafuate taratibu na kanuni za usalama barabarani.

“Kuendesha pikipiki imekuwa sehemu kubwa sana ya kuvunja sheria kwa sababu waharifu wengi wanatumia pikipiki, hivyo tumewapa mafunzo hayo ili waweze kuwabaini waharifu na kuwajengea uwezo wa wao kutoa taarifa ili sheria iweze kuchukua mkondo wake”.Amesema Mkuu wa Usalama barabarani Solomoni Mwangamilo

Halmashauri ya Jiji la Tanga imetenga jumla ya Tshs 800,449,700/=kwa ajili ya mikopo kwa wanawake,walemavu,na Vijana ,ambapo vijana wametengewa jumla ya 355,094,000 /= na hadi kufikia juni 2019 jumla ya Tshs 353,000,000/= zimetolewa kwa vikundi 20  vya vijana wa Jiji la Tanga .

Baadhi ya Vijana wakiwa kwenye Pikipiki walizokabidhiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela akiwa amekaa kwenye Pikipiki.

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ndugu Daudi Mayeji akiongea katika makabidhiano ya Pikipiki hizo.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.